Imani


Jambo la kwanza kuuliza wewe unaye soma karatasi hii, nikwamba je umkristo? Neno mkristo maana yake ni kua kama Kristo (Matendo 11:26). Je unafanya mambo katika maisha ambayo Kristo Jesu aliyatenda katika maisha yake? Alienda kila mahali akitenda mema, akiwaponya wote waliofungwa na shetani.

Je lengo lako na nia ya ko ni nini maishani? Ni jambo la maana sana nia yako ku a sawa, ama unayo yatenda yasiwe sawa, hata yakiwa mazuri namna gani. Je nia yako nikua na nyumba, ama ngari, ama pesa yako kwenye banki, ama nia yako nikua na biashara, sifa kujulikana, au mamlaka ya ulimwengu huu? Rafiki yangu haya ni maono mabaya sana Kama ungali kua tayari kuliko wote na mwenye sifa kuu, na mwenye mamlaka na nguvu ulimwenguni, ingali kua tu ubatili na upotovu wa roho. Mfalume Sulemani katika bibilia alikua na vitu hivi vyote, bali aliviita ubatili.

Kupata neema na Mungu ndiyo hazina ya kweli inayo dumu. Kupata elimu ya juu kuhusu vitu vyote maishani ni bure, maana yale yaliyomo ulmwenguni yata kwisha kwa wakati mfupi hivi, na hayatakumbukwa kamwe. Tunapo ongea juu yakujitayarisha kwa wakati ujao, je wakati ujao uko wapi? Si uko na Mungu. Yeye ameshikilia moyo na ufalume mikononi mwake, na anaigeuza kokote apendako, kama mito ya maji bibilia yasema. Aumba wema na wabaya na ana njia yake kati yao, kulingana na maandiko.

Hakuna tumaini katika ulimwengu huu, ama ulimwengu ujao bila Mungu. Niliongea na muhuduma siku moja juu ya maisha yake yajao. Alikua akipanga kumutumikia Mungu mara tu atakapo maliza kulipa nyumba yake, na alipokua akimaliza malipo ya kwanza, mtoto alizama kwenye ziwalililokua nyuma ya nyumba yake. Ingali kua vizuri kama angali peana mambo yake yote kwake Mungu, hapo mwanzo.

Mtu alikuja kwa mukutano wetu jioni na Roho wa Mungu alipo kua akivuta mioyo kutubu alipewa nafasi kukubali wokovu bali akakataa. Siku iliyo fuata katika matanga kwenye kijiji kimoja mchana niliangalia uso wake uliyo kua umekufa ukiwa ndani ya geneza. Kifo kilimpiga upesi baada yakumkataa Mungu Hakuna amejitayarisha kwa maisha yajao baada ya kifo. Katika mukutano mwingine niliwaomba watu wawili waje na wakakataa, mara hivi, watu hao wawili wakafa. Nina weza kuchukua wakati mwingi kueleza mambo yote ambayo yametukia katika huduma yangu, yakidhibitisha kwamba hakuna uzima bila Mungu.

Hakuna amani kwa mtu mwovu bibilia yasema. Kunayo sauti ya kilio kwa masikio ya tajiri na hiyo sauti haina kikomo. Kusumbuliwa na uonga wakupotenza mnao wapenda, mangonjwa, kukosa fahamu na mabaya katika maisha ni njia mbaya yakuishi. Kujaribu kumaliza ukosefu wa pesa, naukosefu wa mali ambayo tunaifanyia kazi kwa nguvu na kuwatesa wenzetu kwa njia zisizohaki si uzima. Maisha ya unafiki ya wa kristo kujidangaya wenyewe kila siku kwa akili zetu wenyewe tukioyesha imani na tumaini ambayo haipo ndani ya mioyo yetu. Je hii ni maisha?

Nia yetu kwakuwatumikia wenzetu lazima iwe ile yakuhusika sana na wenzetu na kuchukuwa jukumu ya kua mutunzaji wa ndungu yako. Kila mmoja wetu anategemea aina moja ya kitendo fulani kutoka kwa mwenzake. Mungu ameiweka hivyo ili tuwe watunzaji wa ndungu zetu. Kaini alimuuwa Habili ndunguye na akakataa kua mutunzaji wa ndunguye. Kwa kuji anganya mwenyewe Mungu atamlipia mtu kulingana na jinsi alivyo. Apataye utajiri na mali kwa njia ya undanganyifu ata katiliwa mbali na siku zake, na mwishowe atakua mjinga maandiko yasema hivyo.

Usitumainie tu nyumba nzuri, mavazi mema, na mangari ambayo unaona watu wakiwa nayo. Usitumainie tu sifa na cheo na mamlaka katika maisha yako. Bali tizama fikiria pia vio vya wenda wazimu vyumba vya kutibu wenye ungojwa wa kifua kikuu, hospitali na habari ya kila siku ya magazeti na maovu yote ya ulimwengu kama makelele ya vingora inayo sikika kila mara mijini. Mambo hayo ya kuogovya yana nionyesha kwamba maisha ina mengi zaidi ya raha tu ya mambo ya anasa. Kuna mahali pema pa juu pa kuishi ambako tuna furaha amani na haki. Kumutumikia Mungu kuleta mambo haya.

Hiyo sauti ya maombi abayo imeitana kupitia karne zote bado ina kuita wewe na mimi, Ni sauti ya Mungu kupitia huduma na watoto wa Mungu wakiwaomba watu waje tangu ulimwengu ulipo anza. Sauti ya Kristo ilijiinua katika vizazi vilivyo pita na ilipasa sauti siku za Noah kabla ya uharibifu. Imepasa sauti katika siku za Kristo Yesu kabla ya uharibifu kuangukia Jerusalem. Ilinena kwa watu walipo panda milima wakitafuta kivuli kutokana na dhoruba ya maisha katika Historia ya miaka ilioyo pita ikaja sauti nyororo ya yule mtu mugalilaya aliye ishi maisha ya upweke kwa ajili yako na mimi. Leo sauti hiyo hiyo bado ina ita ikiomba ulimwengu huu wakisos holisiti umurudie Mungu. Na kuuliza swali rafiki yangu mbona tusiitikie mwito huu wa kutubu tukingeukia Mungu na kuacha njia ya anasa na majivuno na mambo makuu lakini tugeukie nakushugulishwa na watu wanyonge, na wadhaifu.

Yesu alisema kwamba kizazi hiki cha mwisho kituakua na watu wamajivuno, wakiburi wanao jipenda wenyewe kuliko Mungu. Paulo alisema hawa ndiyo watu ambao mwisho waulimwengu umewafikia. Wengi wenu ambao nina ongea nao wameziba thamiri yao na imepaswa na chuma ya moto na hawawezi kusikia kwani ametoa Roho zao kwa shetani kutenda mambo maovu.

Tukiona kwamba kila kitu ulimweguni kita chomwa na ulimwengu uta chomwa pia Petro akiuliza je inatupasa kua watu waaina gani katika mweneo ido mutakatifu na utawa mukitzamia hata ije siku ya Mungu.

Petro huyu ambaye alipewa funguo za ufalme siku ya petecoste kanisa lilipo zaliwa siku ya kwanza watu elfu tatu waliingia katika kanisa la kwanza. Kati ya watu bilioni bili na nusu na bilioni tatu katika u limwengu wa leo ni wangapi wataisikia sauti hii ya Kristo inapo paswa kupitia kinywa cha ke kuingia ulimwenguni.

Mwito ni kutubu kubatizwa katika jina la Yesu Kristo upate ondoleo la thambi ili uweze kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa maana ni kwako wewe na watoto wako na kwa wengi ambao Bwana wetu na Mungu wetu atawaita. Wewe ni kati ya mwito huu?

Bibilia husema kwamba watu hawa waliendelea kila siku kwa muoyo mmoja kwa mafudisho ya mitume, kumbuka hakuna njia ingine.

Kwa neema kupitia imani tumeokolewa, si kwa kazi zetu mtu asijivune. Lakini ni karama ya Mungu. Walisikia neno Petro alihubiri waka amini neno na imani inayo kuja kwa kusikia neno la Mungu ilidhihirishwa kwa maisha yao kwa kutii neno la Mungu ambalo Petro alinena. Walipokea ubatizo wa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu wa milele, wokovu na nguvu za ufufuo mara tu walipo amini.

Ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahim ndani ya Kristo ilitimizwa siku ya petecoste Petro alipo sema, “ahadi hii ni kwa watu wote ambao Bwana Mungu wetu atawaita. Tumeambiwa tufanye mwito wetu na choguo letu kua sawa”. Tutatambua aje kwamba tuko katika mawazo ya mbele ya Mungu? (I Petro 1:2) inatuambia kwamba sisi tumechaguliwa na p ia sisi ni wateule wa Mungu kulingana na mawazo ya Mungu kupitia kutakasika kwa Roho na kwakutii na kwa kunyunyiziwa Damu ya Jesu Kristo. Mungu ametupatia vitu vyote ambavyo ni vya uzima na uungu na ametuitia utukufuni. Ambako tumepewa ahadi kuu na kwa haya muwe washirika wa utawa walioepuka na maovu yalioko ulimwenguni kwa sababu ya tamaa. Katika msitari wa tano ina tuweleza kwamba tujitahidi sana katika imani yetu tu weke wema na katika wema maarifa na katika zaburi utauwa na katika utauwa upendo wa ndungu na katika upendo wa ndungu upendo. Vitu hivi vikiwa ndani yako hautakua mtu asiye zaa matunda lakini asiye na vitu hivi yeye ni kipovu na hawe zi kuona mbali na amesahau kwamba alioshwa kutoka kwa dhambi zake za kale.

Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hautakabali, haukosi kua na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mambaya hauufulahii udhalimu. Bali hufulahia pamoja na kweli huvumilia yote, huamini yote, hautumaini yote, hutumaini yote, huustahimili yote. Jesu alisema tutawatambua wakristo kwa matunda wanayo zaa tumepita kutoka kwa, mauti kuingia uzima kwa sababu tunapendana kama wandungu. Mungu ni upendo akaaye ndani ya upendo, anakaa ndani ya Mungu. Matunda ya Roho ni, upendo, furaha, amani, ufumilifu, utuwema, fadhiri uwaminifu, u pole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Mambo haya yanadhibitisha wewe umeitwa na kuchanguliwa kama yataoneka katika maisha yako.

Je hamjui ya kwamba watendao maovu hawatauridhi ufalme wa Mungu. Msidangaywe washerati hawatauridhi ufalme wa Mungu, wala walawiti, wala waabudu sanamu, wala wazizi, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyanganyi hawata urithi ufalme wa Mungu. Paulo alisema msidhulumiane.

Lihubiri neno uwe tayari wakati ukufao na wakati usiokufaa, karipia, kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapo yakataa mafundisho yenye uzima ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe. Watajipatia walimu makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli. Nakuzingeukia hadithi za uongo. Mtu yeyote akifundisha mambo mengi kando ya mafudisho haya na kama si ya utawa wa Mungu yeye anan kiburi hajui lolote ana maswali ya upumbavu yanayo leta faraka na mawazo ma ovu hakuna mwenye haki hata mmoja na kama kordoo tumepotea kila mmoja, wote amengeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi zote. Alipigwa kwa sababu ya makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupingwa kwake sisi tumepona.

Nina ongea juu ya imani iliopeanwa kwa watakatifu, amini bwana Jesu Kristo leo uokolewe. Bwana akubariki ndiyo maombi yangu.

Imeandikwa na Rev. George Leon Pike Sr.

Yeye alianzisha “Jesus Christ’s Eternal Kingdom of Abundant Life, Inc.”

Utakatifu Kwake Mungu

Ujumbe huu umeandikwa kwa kupeana bure bila malipo yoyote. Kwa nakala zaidi andika kwa kingereza ikiwezekana kwa anwani iliyoko chini ukieleza ni nakala ngapi unaweza kutumia vizuri.

SWA9915T • SWAHILI • THE FAITH