Neno La Mungu La Uponyaji


Kwa wote ambao hawajafurahia uzima tele-tele wa Mungu.

Jambo la kujua ni kwamba Mungu ni Roho katika uzima. Ndani yake hakuna kifo. Shetani ni roho wa kifo, na ndani yake hakuna uzima. Mungu amepeana uzima wa muda na wote ni washiriki wa uzima huu ambao wamezaliwa ulimwenguni. Tuna pumua na kufurahia pumzi nzuri ya uzima. Je uzima unaweza kua mzuri jinzi gani? Kwa wale hawana shaka na mawazo ya pingamizi. Je ni vizuri namna gani kutembea barabarani kuendesha gari na kuona maua viumbe na uzuri wa maumbile yao! Mungu akiviwekea mkono wake. Kua na afya nzuri katika mwili wako na bila mawazo ya hofu ama kujisikia ukiwa mgonjwa. Mawazo yako yakipitia rohoni yakileta furaha teletele.

Kweli imesemwa vyema na mwandishi kwamba tunateka maji kutokana na chemi chemi ya wokovu kwa furaha (Isaya 12:3). Tuiingie mlangoni pake kwa shukrani na nyumbani kwake kwa kusifu (Zaburi 100:4). Bibilia inatuambia aliye na moyo wa furaha ni mzuri kama dawa lakini moyo uliyo vunjika hukausha mifupa(Mithali 17:22). Tumeambiwa na mwandishi, huzuni huleta kifo. Mtu yeyote anaweza kuona wazi kwa nini bibilia inafundisha kwamba kumtumikia Mungu ni furaha, amani, na haki ndani ya Roho Kwa sababu imani ndani ya neno la ahadi katika maandiko yake yasio pikisika na kupeperushwa, na neno lake lisilo shindwa ambalo halibadiliki huleta uzima wa milele.

Ni maneno ya upako na pumzi ya uzima. Ahadi ya tumaini na msamaha na, kuacha yeyote atakaye na aje. Ni ahadi ya uponyanji kwa wote. Kulingana na imani yako na iwe hivyo kwako bila upendeleo wa watu lakini ukiwachukua watu wote kama viumbe vya Mungu. Sisi huamua mwisho wetu.

Je mtu anaweza kufurahia aje uzima wote? Kunayo njia moja tu, Mungu hajatupa roho wa uoga. Hatujazaliwa na uoga lakini ni roho ya pepo ambayo huingia ndani ya roho zetu kupitia njia ya kutoamini neno la Mungu na ahadi zake ambazo zimetumwa na zimetuweka katika uzima.

Yesu alisema, msifadhaike mioyoni mwenu, na pia msiogope. Ni juu yetu kutumia upande mwingine wa uzima kuwa na imani ndani ya neno la Mungu, kama jinsi mawazo yetu yana imani ambayo imetokana na mawazo ya Kristo. Lazima turidhike na Imani ya Yesu Kristo. Paulo alisema “Tuna mawazo yake Kristo” Lazima tuipatie uhuru, kupitia mawazo kuingia mwilini mwako kama wokovu, uponyanji na mengineo.

Ufalme wa Mungu umo ndani yetu. Kwa hivyo uponyaji umo ndani yetu. Paulo alisema sisi tu mwili wa Kristo. Watu kadha wa kadha wame lala Yesu alifanyika magonjwa yako akasumbuka mwilini akafa msalabani, ili wewe uwe mwili wake ambao uko huru kabisa na dhambi na magonjwa. Unafanya hayo kwa imani unapo amini ya kwamba alibadilisha mahali pako na yeye. Wewe unaponywa tu mara moja kila mara kumbuka mwili wako uliokuwa chini ya laana ya torati ya hukumu ya Mungu kwa Musa ilitundikwa msalabani, na kwa sababu wewe ni mwili wa Kristo umewekwa huru kutokana na laana kupitia imani yako ndani ya Kristo.

Ahadi ya Mungu na agano zake zote ziko kwa Yesu Kristo. Tunaipokea kupitia imani ndani ya Kristo kwa kuamini kwamba sisi ni mwili wa Kristo, inafanya hizo ahadi kuwa zetu. Kumbuka imani yetu ni asili ya akili zetu ambayo tunalinganisha na neno la Mungu. Neno la Mungu ni mawazo ya Kristo. Imani inakuja kwa kusikia neno la Mungu. Imani ya Kristo ni mguzo wa ndani ya moyo na roho. Kuamini kwamba tumeokoka na tumeponywa kwa mawazo yetu pekee inamaanisha kwamba tumedanganyika na kupotea. Lazima uwe mguzo wa ndani ya moyo na roho. Kwa moyo binadamu anaamini mambo ya haki na kama jinsi mtu anavyo waza moyoni mwake, ndivyo alivyo. Yesu alisema “Kama mngeamini moyoni mwenu na msiwe na shaka mngelipokea lolote muulizalo.” Moyo hautamani kabisa mpaka uguzwe na kujitoa kwako kwa Mungu. Ndiyo kwa sababu, imani bila matendo imekufa. Matendo huamusha tumaini ndani ya neema ya Mungu wako. Imani ya Kristo ndani yako imewekwa huru kutokana na kufinyiliwa Na kuhisia) hufa kupitia kufunga na kuwa chini ya mamlaka. Shetani hana njia ya kufanya kazi (kama amekemewa kutoka ndani yako) ila kupitia kwa nafsi zako tano ambazo zimeweza kuzuia imani yako. Sasa kwa kusikia na kuelewa mambo haya natujenge imani yetu kwa kusikiza neno la ahadi zake kwetu.

Mungu wangu atatosheleza haja zangu zote kulingana na uwezo wake utukufuni. Kumbuka haja za mwili, za kipesa ama za kiroho yeye atatimiza zote. “Mimi ni Mungu asameheaye maovu yenu yote na aponyae magonjwa yenu yote.” Tazama alisema! Nitatoa magonjwa kutoka katikati yenu” (Nakuikemea itoke kwa roho yako). Mungu ni uzima kama uponyaji, wokovu, amani, furaha, na mafanikio ambayo ni ya roho uzima na mwili wa Kristo, ambaye u’ mwili wake. “Yesu alisema nimekuja ili mpate uzima”. Kuwaza hivi mawazo na imani ya Kristo ni ambayo kupitia yeye umepatikana huo uwezo. “Je, siataweza, pamoja na Kristo kutupatia vitu vyote bure”. Paulo alisema. Roho wa shetani ni mauti na adui wa Mungu. Mambo ya mauti ni uoga, huzuni, kufadhaika, kufa moyo na magonjwa, mambo haya yote ni adui kwa Mungu. Kristo Yesu alikuja kinyume cha mambo haya yote: njaa, kufua kikuu, maradhi, kupofuka, kuwa bubu, kuwa kiziwi, kifafa na magonjwa mengine yote ambayo hayajaandikwa katika kitabu cha torati. Nyinyi mmekombolewa kutokana na mambo haya. Mambo haya yote yalikua chini ya laana ya torati. Nyinyi mko chini ya neema”.

Kila magonjwa na maradhi ambayo yamejulikana ulimwenguni kote yaliletwa na dhambi. Dhambi ilikua kutoamini neno la Mungu. Hawa alitenda dhambi hii. Kila ambacho si cha imani ni dhambi. Adamu alileta watu wote chini ya laana kwa kuto amini. Kristo alikomboa watu wote kwa laana kwa imani. Ndani ya Adamu wote wanakufa, ndani ya Kristo wote wanawekwa hai.

Alituma neno lake (Yesu) na likawaponya. Imani ndani ya neno lake inafanya neno kuwa mwili. Tunafanyika neno na waraka ambayo inajulikana na kusomwa na watu wote. Neno la Mungu lilifanyika mwili. Sisi si umoja na neno kama mwili wa Kristo, hakuna magonjwa ndani ya Mungu. “Kwa mapigo yake tumepona”. Una asili ya Kristo. Walimshinda shetani kwa neno la ushuhuda na damu ya mwana kondoo na kazi ya kalivari. Kukiri kwa maneno na matendo yale aliyowatendea. Usitegemee mawazo yako tu. Amini Bwana (lile neno na moyo wako wote).

Lazima tulete kila wazo chini ya mamlaka ya Kristo, tukitupilia kila aina ya mawazo mabaya, uoga na shaka tukiharibu mawazo mabaya ambayo ni adui wa Mungu. Mungu atabadilisha kila ambacho kimenenwa kutokana na kinyua chake. Atatunza neno lake na kulitenda.

Kama ni kwa mapigo yake tumeponywa, naye hana upendeleo na tutaviitia vile vitu ambavyo haviko na vitu ambavyo viko kama vile haviko. Wenye haki wataishi kwa imani si kwa vile vitu tunavyo ona. Basi imani yako imekuponya.

Mungu anatuambia kwa neno lake, “Kwaraba nitafanya juu ya mambo yote uendelee na ufanikiwe”. Mafanikio yako kwa kazi yako ya roho. Ni Bwana Mungu wako apeanaye nguvu za kupata utajiri. Lazima upeane utajiri na mali yako kwa kazi ya Mungu ili upate utajiri wa milele. Amini (kumbuka hali yako ya moyo) kwamba magonjwa yako hakika na kweli yameondoka hayawezi kurudi tena. Unaweza kuamini kweli mwili wako utaongozwa na kulazimika kutenda mambo ya haki, na matendo ya kudhibitisha. Mungu hawezi kutuachilia ama kututoroka. Uliza kwa imani bila kuwa na shaka Yesu alisema. Yohana alisema, hii ndiyo tumaini yetu ndani yake lolote tuulizalo katika jina lake tunapokea. “Mioyo yetu isipo tuhukumu basi tunatumaini ndani ya Mungu”. Paulo alisema “na kujaribu kuweka dhamiri yangu isiwe na mawaa kwake Mungu na binadumu”. “Kila moja aulizae hupewa” andiko la sema “lolote uulizalo katika jina langu nitatenda”. Yesu alisema tumtukuze aliyeko mbinguni. Uliza, “ili furaha yako ijae”. Alibeba magonjwa yako na huzuni ndani ya mwili wake kwenye mti. Na, “kwa mapigo yake tumepoywa”. Yesu alisema imemalizika kama alizibeba mwilini mwake badala yako. Mbona uzibebe tena? Kwa sababu ya uongo wa shetani.

Kumbuka imani ni mfano wa kutoa mawazo yako yote na lengo lako kwake. Kuamini neno lake nikujikanya mwenyewe kutoka kwa mawazo yako na moyo wako, na kuwa mawazo imara ya ahadi zake itatokana na mawazo imara ya ahadi zake, naitaleta furaha afya na mafanikio kwako ukiachilia kuamini inawacha kufanya kazi. Kila mara chunguza mawazo yako na jinsi unavyo jisikia. “Badilisheni nyinyi nyote kwa kuweka upia akili zenu”. Ichangamushe mawazo yako ilio Safi mawazo ya Kristo na udhibitishe kile ambacho ni chema na kimekubalika, yeye ni kuhani mkuu. Ameguzwa na udhaifu wetu. Akiwaombea mioyoni mwenu kuhani mkuu wa toba yenu. “Kwa moyo binadamu anaamini haki na kukiri kwa wokovu kuna nenwa na kinywa”. kiri, amini, na upokee na upone katika jina la Yesu Kristo kutokana na udhaifu, unyonge, mangonjwa na kushindwa. Mungu akubariki ndilo ombi langu.

Imeandikwa na Rev. George Leon Pike Sr.

Yeye alianzisha “Jesus Christ’s Eternal Kingdom of Abundant Life, Inc.”

Utakatifu Kwake Mungu

Ujumbe huu umeandikwa kwa kupeana bure bila malipo yoyote. Kwa nakala zaidi andika kwa kingereza ikiwezekana kwa anwani iliyoko chini ukieleza ni nakala ngapi unaweza kutumia vizuri.

SWA9908T • SWAHILI • GOD’S HEALING WORD